Products

House Help App Membership

House Help App Membership

10,000.00 TZS
10,000.00 TZS

HouseHelp App ni suluhisho jipya la kidigitali linalokusaidia kupata au kuajiri mfanyakazi wa nyumbani kwa urahisi, haraka na kwa usalama.

Mara nyingi familia hukaa na changamoto ya kutafuta msaidizi anayeaminika, huku vijana wengi wakitafuta kazi bila mafanikio. Sasa kupitia app hii, familia hupata msaada bora ndani ya dakika chache, na wasaidizi hupata ajira zenye mikataba ya heshima.

Ni rahisi kuanza kutumia. Hatua ya kwanza ni kubonyeza "Buy Now" na kufanya malipo ya TZS 10,000/= pekee, kwa njia ya MPesa, Airtel Money au Mixx by YAS, na kulipia moja kwa moja Online.

Baada ya hapo, utaweza kuona orodha ya wadada wanaotafuta kazi, majina yao, mahali wanapotoka, uzoefu wa kazi, kiwango cha mshahara, na mawasiliano yake. Na dada wa kazi anayetafuta kazi anaweza kujiweka kwenye orodha, pia anaweza kuchagua familia iliyojiweka kwenye orodha ya familia zinazo tafuta wasaidizi wa kazi za nyumbani.

Mfumo wetu unawaunganisha wote kwa kutumia teknolojia ya “matching” inayohakikisha kila familia inapewa msaidizi anayefaa mahitaji yao. Kwenye App hii kuna Mkataba wa kazi unaoeleza majukumu, muda wa kazi na malipo, hivyo kuondoa makubaliano ya maneno ambayo mara nyingi husababisha migogoro.

Pia app ina sehemu ya ratings na reviews ili familia na wasaidizi waweze kushirikiana kwa uwazi na kwa kuaminiana zaidi.

Kwa kifupi, HouseHelp App ni kama Bolt kwa ajili ya wasaidizi wa nyumbani, ila imebuniwa mahsusi kwa changamoto za kila siku zinazotukabili. Badala ya kuhangaika kuuliza jirani au kutumia madalali wasio na uhakika, sasa unaweza kupata suluhisho moja la kidigitali lililo salama, rahisi, na linaloleta heshima kwa kila upande. Pakua app leo, jisajili na anza safari ya kupata msaada sahihi au ajira ya ndoto zako.